TANGAZO

KWA WALE WANAOHITAJI T.SHIRT KWAAJILI YA SARE SIKU YA AMBAYO WASANII WATAJUMUIKA KWA PAMOJA SIKU YA KWENDA MAHAKAMANI WAFIKE BAJOMBA CO.LTD MAGOMENI MOROKO HOTEL AU WAPIGE SIMU NAMBA:0715316796. BILA KUSAHAU MCHANGO WA TSH. 2000/=

SPORTS

                               

David Moyes kocha mpya wa Manchester United



Uongozi wa Old Trafford umetangaza rasmi na kuthibitisha kuwa David Moyes atakuwa meneja mpya wa timu hiyo kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson atakayestaafu mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Old Trafford mchana wa leo, David Moyes amepewa mkataba wa miaka sita wa kuifundisha Manchester United kuanzia msimu ujao.


                                SIR ALEX FERGUSON ATANGAZA KUACHIA NGAZI.

Sir-Alex-Ferguson
Kocha mashughuli wa timu ya ligi kuu ya Uingereza, Manchester United, Sir Alex Ferguson ametangaza kustaafu baada ya kufanya kazi na timu hiyo kwa zaidi ya miaka 30, club hiyo imetangaza leo. Sir Ferguson atastaafu rasmi mwisho wa msimu huu, ambao utakuwa wa 27 kama kocha wa timu hiyo. Atamaliza kama kocha mwenye mafanikio kuliko wote katika historia ya soka ya Uingereza.  Ferguson mwenye miaka 71 hivi sasa amefanikiwa kusimamia timu hiyo yenye mamilioni ya mashabiki tangu mwaka 1986
katika miaka 27 aliyokua kama manager wa timu hiyo, Sir Ferguson ameshinda vikombe 30, ikiwamo vikombe vikubwa 13
Ferguson ataachia nafasi hiyo baada ya mechi ya mwisho ya club hiyo kwa msimu huu ambayo itakuwa ni mechi kati yao na Manchester City.
Haijajulikana bado nani atakae mrithi kiti hicho