Muigizaji Batuli amekanusha vikali uvumi ulionea kwenye baadhi ya vyombo vya habari kua ni muathirika wa ugonjwa wa Kansa. Hata hivyo Batuli alisema ni kweli aliwahi kupata uvimbe kwenye ziwa lake la kushoto lakini ilikua ni uvimbe wa kawaida na alishafanyiwa upasuaji na alipofanya uchunguzi haikua ni Kansa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari. "Kwanini hawa watu wa habari hawapendi kuchunguza kitu kwa kina au kumuuliza muhusika ili kupata ukweli wa jambo, wao hua wanaandika tu wanavyojisikia? Mimi sina Kansa na namuomba Mwenyezi Mungu sana aniepushie na maradhi kama hayo." Alizungumza Batuli.
0 comments:
Post a Comment