Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunisaidia kunifanikishia kazi ya kuadhimisha mwaka mmoja baada ya kifo cha Kanumba, naishukuru Clouds Media Group chini ya Mkurugezi Rughe Mutahaba aliyesimamia kwa kiasi kikubwa sana shughuli ya jana ambayo mimi mwenyewe ikua ni kazi kubwa sana lakini kwake imekua ni ndogo sana, kiukweli Mwenyezi Mungu ambariki na amzidishie baraka tele na mafanikio tele.
Pia nawashukuru Watanzania wote waliojumuika nasi pale Ledears Club na waliokua wakifuatalia kwenye Clouds Tv wote nawashukuru, na wale wote waliotakakujumuika nasi lakini wakashindwa kwa namna moja au nyingine pia nawashukuru pia.
Naishukuru pia Familia ya mama Kanumba kwa tuzo walizoandaa kwa watu mbalimbali kama shukrani zao kwa wengine. Napenda kuwaambia Watanzania wenzangu kua Filamu yangu ya ''AFTER DEATH'' tuliyoionesha pale Ledears Club, itakua madukani nchini kote hivi karibuni. Nawaomba Watanzani waniunge mkono kwenye hilo.
Monday, April 8, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment