TANGAZO

KWA WALE WANAOHITAJI T.SHIRT KWAAJILI YA SARE SIKU YA AMBAYO WASANII WATAJUMUIKA KWA PAMOJA SIKU YA KWENDA MAHAKAMANI WAFIKE BAJOMBA CO.LTD MAGOMENI MOROKO HOTEL AU WAPIGE SIMU NAMBA:0715316796. BILA KUSAHAU MCHANGO WA TSH. 2000/=

Wednesday, November 16, 2011

NAJUA KAMA MIMI NI MLEMAVU LAKINI SIWEZI KUBWETEKA - THOMAS.

Bwana Thomas mkazi Ubungo jijni Dar-es-Salaam ambaye ni kabila la Wamasai wa moani Arusha amekua akijipatia fedha kwa staili ya aina yake anapokua akiendesha Baiskeli yake ambayo pia huitumia kama usafiri wake wakutembelea. Bw.Thomas ambaye amekua na ulemavu wa miguu tangy kuzaliwa kwake amesema yeye hakubahatika kupata elimu yoyote lakini  anamshukuru Mungu amekua akimpa pumzi na nguvu kila siku ya kutafuta pesa kama watu wengine wasio na matatizo kama yake. "Kiukweli mimi kuhusu swala la utafutaji sina tofauti na watu wengine wanaoamka hasubuhi na kwenda mahofisini maana wote mwisho wa siku tunasaka kipato." Bw.Thomas aliyasema hayo huku akitabasamu.

Amekua akijiingizia kipato chake kwa kuomba lakini wakati mwingine watu hufurahishwa na uendeshaji wa Baiskeli na kuamua kumpa kipato ambacho ndicho kinachoendesha maisha yake ya kila siku.

Bw. Thomas akishuka kwenye Baiskeli yake kwaajili ya kujipatia msosi wake wa mchana.


Bw. Thomas (kulia) akiwa na mdau wangu mkubwa Bw. Gaston Kissombe wakipata chakula cha mchana maeneo ya Magomeni.

Thomas ameshakula anajiandaa kuondoka na kuendelea na mishemishe.

Akiwa safarini kwenye kujitafutia kipato.

Thomas akielekea maeneo yake ya kazi kutokea Ubungo..

0 comments:

Post a Comment