TANGAZO

KWA WALE WANAOHITAJI T.SHIRT KWAAJILI YA SARE SIKU YA AMBAYO WASANII WATAJUMUIKA KWA PAMOJA SIKU YA KWENDA MAHAKAMANI WAFIKE BAJOMBA CO.LTD MAGOMENI MOROKO HOTEL AU WAPIGE SIMU NAMBA:0715316796. BILA KUSAHAU MCHANGO WA TSH. 2000/=

Friday, November 25, 2011

TUNAPOSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU TUWAKUMBUKE NA HAWA...

Kiukweli tupo wenye maisha nafuu, wapo wenye maisha mazuri na wapo ambao kila siku ni afadhali ya jana. Watoto hawa wa mtaani walinihuzunisha sana nilipowakuta maeneo ya FIRE KARIAKOO, wakiomba fedha kwaajili ya kujikimu na mahitaji yao ya kila siku, lakini kilichonihuzunisha zaidi ni kwamba wao ndio watunza familia kwa mujibu wa wao wenyewe kwa kusema lkuwa mama yao ni kipofu na baba yao alishafariki miaka mingi iliopita.

Watoto hawa waliponiona tu walikuja mpaka dirishani mwa gari langu, walipa huzuni sana. Naiomba Serekali katika kusherekea miaka 50 ya Uhuru, iwakumbuke na watoto hawa wa mitaani kama ilivyofanyika kwa wahanga wengine kama Gongo la Mboto, Mbagala na kwingineko.

Naye akiomba msaada....

Wanasubiria foleni ikianza ndipo na wao waanze kuomba.

0 comments:

Post a Comment