TANGAZO

KWA WALE WANAOHITAJI T.SHIRT KWAAJILI YA SARE SIKU YA AMBAYO WASANII WATAJUMUIKA KWA PAMOJA SIKU YA KWENDA MAHAKAMANI WAFIKE BAJOMBA CO.LTD MAGOMENI MOROKO HOTEL AU WAPIGE SIMU NAMBA:0715316796. BILA KUSAHAU MCHANGO WA TSH. 2000/=

Wednesday, October 17, 2012

VURUGU ZANZIBAR ZAIBUKA TENA.

Baadhi ya vitu vikichomwa na kuharibiwa vibaya.
Wengine wakiwasiliana na ndugu na jamaa kuwajulisha hali halisi.
Polisi walifika eneo la tukio kuhakisha amani inapatikana. 
Vurugu zimeibuka Zanzibar, inasemekana kufuatia kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la Uamsho linaloendesha mihadhara ya dini ya Kiislam na kampeni za kuvunja Muungano, Sheikh Farid. Askari wa kutuliza ghasia wanapiga mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa kundi hilo ambao wanachoma matairi na kurusha mawe kwa askari.
      Inasemekana vurugu hizo zimefikia kiwango cha kusababisha barabara za eneo la Darajani mjini Unguja, kufungwa. Wafuasi hao wa Uamsho wanaandamana kushinikiza polisi wamwachie huru kiongozi wao huyo. Chini ni baadhi ya picha ya kilichotokea mchana huu huko. Picha zote kutoka: afrokija.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment