Thursday, March 14, 2013
DYANA KIMARO (MIKOGO) CHUPU CHUPU KWENDA SERO.
Alipofika eneo husika (location) Dyana alitaka kupewa chake kabla ya kuanza kupiga picha ndipo mtayarishaji huyo 'OMARY' akamwambia maswala yote ya hela amuone jamaa mmoja anayeitwa Gaston Kissombe ambaye alikua ni location manager na pia ni Production manager wa kazi hiyo. Ndipo kijana huyo akamjibu unayetakiwa kucheza nawe kapata tatizo, kama utaweza nakupa nauli urudi nyumbani halafu kesho hasubuhi tutakuja kukuchukua, Dyana akakubali lakini akasema ni vizuri mnirudishe nyumbani kwa gari la Production. Gaston almaarufu kama Liumba akambeba mpaka kwao ambapo alipokaribia kufika maeneo ya kwa akina Dyana, Dyana akataka kupewa hela nusu ya makubaliano aliyokubaliana na Bw. Omary, ambapo Omary alimjibu ni mpaka siku inayofuata lakini Dyana hakuelwa na kuanza kufanya fujo kwenye gari na kugoma kushuka kwenye gari ndipo Dyana akataka kurudishwa mpaka kambini maeneo ya Buguruni, na baada ya kufika kambini ndipo Dyana akaamua kufanya fujo kwenye hotel ya watu na kujifanya kapandisha mashetani na kumkunja na kumpiga mpiga picha anayejulikana kwa jina la Msekwa, na ndipo Msekwa akamwambia kama wewe unajifanya umepandisha masheatani basi mimi 'MSEKWA' ndiyo shetani mkuu na leo ndiyo utanijua. Msekwa ndipo akaamua kumkamata na kumpeleka polisi Dyana, Dyana bila kujua aliyekua anamfanyia fujo ni mtu wa usalama. Wakiwa njiani kuelekea polisi Dyana akagundua kuwa kweli Msekwa yuko serious na atampeleka kweli ndipo Dyana akaomba radhi na kuahidi kufanya kazi hata bure.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment