TANGAZO

KWA WALE WANAOHITAJI T.SHIRT KWAAJILI YA SARE SIKU YA AMBAYO WASANII WATAJUMUIKA KWA PAMOJA SIKU YA KWENDA MAHAKAMANI WAFIKE BAJOMBA CO.LTD MAGOMENI MOROKO HOTEL AU WAPIGE SIMU NAMBA:0715316796. BILA KUSAHAU MCHANGO WA TSH. 2000/=

Tuesday, March 19, 2013

MAPEDESHEE TUMIENI VIZURI PESA ZENU.

Napenda kutumia fursa hii leo kuzungumza kitu fulani kidogo tu ambacho nimekiona mimi, mara nyingi nimekua nikisikia kwenye nyimbo nyingi za wanamuziki wa Tanzania hata wa maeneo mbali mbali kama Jamuhuri ya watu wa Congo wakiwataja watu flani flani ambao inaaminika na watu wenye kipato kikubwa kifedha au huwa wanawasaidia kimuziki hata kimaisha wakati mwingine. Kinachonishangaza kwanini wanapenda kuwatunza kwenye majukwaa tuu? Hao wanaojiita mapedeshee wanaopenda kutajwa kwenye nyimbo za hao wasanii. Nawaomba mapedeshee waende kwenye vituo vya kulea watoo yatima na kutoa misaada ya kifedha na Inshalah Mwenyezi Mungu atawazidishia.

0 comments:

Post a Comment