TANGAZO

KWA WALE WANAOHITAJI T.SHIRT KWAAJILI YA SARE SIKU YA AMBAYO WASANII WATAJUMUIKA KWA PAMOJA SIKU YA KWENDA MAHAKAMANI WAFIKE BAJOMBA CO.LTD MAGOMENI MOROKO HOTEL AU WAPIGE SIMU NAMBA:0715316796. BILA KUSAHAU MCHANGO WA TSH. 2000/=

Tuesday, April 2, 2013

KANUMBA DAY NAJA NA FILAMU YA KUMUENZI.

   Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa hiki nilichokifanya mimi, pia nawashukuru wale wote waliokua nyuma yangu mpaka kufanikisha kufanya Filamu hii ya kumuenzi Marehemu Steven Kanumba. Kiukweli hata ninapoandika habari hii machozi yananitoka kwa huzuni mkubwa sana, na hata mara baada ya kumaliza kutengeneza Filamu hii, wakati nairudia kuingalia ilikua ikinitoa machozi sana maana nilikua naona kama Kanumba bado yuko.
   Nimeamua kufanya Filamu hii kama kumuenzi maana ni Msaani ambaye nampenda na pia naheshimu alichokua akikifanya alipokua hai. Pia napenda kuwakumbusha pia Watanzania wote kuwa Filamu hii si yangu bali ni yao, na ndiyo maana nimeamua kuionesha pale Ledearz Club tarehe 7/4/2013 siku ya Kanumba Day, bila malipo yoyote kabisa.
   Tutaanzia kanisani, kisha tutaenda kaburini kuhani pamoja na familia halafu baada ya hapo tutaelekea viwanja vya Ledearz ku-preview.
   Namshukuru Mwenyezi Mungu kuweza kunifanikishia hili na nawashukuru Watanzania wote na wale Mashabiki wangu pia.
   
     


0 comments:

Post a Comment