Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa Jina la Shirima ambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo
jijini
Dar es Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo
Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa
uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.
Mfanyabiashara
huyo alijirusha toka ghorofani na kuangkia katika Gari aina ya Toyota
Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo,chanzo cha
kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.
Mashuhuda
wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa
na mshtuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia
gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni
mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.
|
0 comments:
Post a Comment