Hemed Suleiman, a.k.a. Phd, juzi ametamka kwa kinywa chake mwenyewe kua Filamu zinamlipa sana kuliko muziki anaofanya. Hemed ambaye ni Mwanamuziki na Muigizaji pia, amesema Muziki ni kipaji chake na ni kitu ambacho anakipenda toka moyoni ila Filamu ni kitu ambacho kilimjia tu baadaye lakini Filamu zimekua zikimlipa zaidi kuliko muziki.
''Kiukweli movie ni tamu sana ukizingatia kila siku niko locations napiga vimeo lakini muziki aliye juu ndio anapata mashavu kila siku.'' Ilikua ni kauli ya Hemed Suleiman akiwa katika utengenezaji wa filamu yake ya Stellah inayotarajiwa kusambazwa na Steps ambapo amemshirikisha swaiba wake mkubwa Gelly wa Rhyms.
Tuesday, May 21, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment