Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu
Mkuuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Sympho Mukandala
amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.
Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya
kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo
hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi
tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao. Iweje
leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa
ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala.
Habari za kuaminka zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji
Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia
uamuzi wake huo.
|
0 comments:
Post a Comment