Icon wa Muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul Juma 'DIAMOND PLATNUMZ' amewashukuru Watanzania wote kwa kumpatia tuzo mbili ambazo zote alishiriki na zote amepata. Pia Diamond ametoa ufafanuzi wa uvumi unataka kuenea kua alisusa kwenda kupokea tuzo na badala yake alimtuma mtu kitu ambacho amekisema si ukweli hata kidogo. Akitoa ushahidi kwa njia simu, Diamond anasema hakuwepo kabisa Dar-es-Salaam. ''kiukweli nilitamani sana kujumuika na Watanzania wenzangu lakini nilikua mbali nikifanya tamasha huko nawaomba radhi sana Watanzania kwa kutokuwepo kwenye tukio la utoaji tuzo.'' |
Thursday, June 13, 2013
DIAMOND ATOA TAMKO KWANINI HAKUWEPO KWENYE TUZO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment