Mwana FA anafikiria kuahirisha shoo yake ya kesho iliyopangwa kufanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na tayari ameanza kuwasiliana na meneja wake kwa ajili ya hatua hiyo.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Mwana FA kuahirisha shoo yake, awali ilipaswa kufanyika Mei 31 mwaka huu lakini ikaahirishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa msanii mwenzake wa Bongo Fleva Albert Mangwea.
Hata hivyo Mwana FA ametoa tahadhara ya kejeri juu ya hatua hiyo huku akimtupia madongo mhasimu wake mkubwa Mwanadada Lady Jay Dee, katika taarifa yake aliyoitupia katika mtandao wa kijamii wa Facebook Mwana FA alisema kwamba,
- "Msiba wa mwana HIPHOP mwenzetu Langa unanifanya nifikirie kuahirisha show ya kesho. Nawasiliana na manager wangu kisha nitawajuza ,but si kwa kumuogopa mwanamke,Let it be clear" alisema Mwana FA.
0 comments:
Post a Comment