Galacha wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Juma, Diamond ameingia tena vinywani mwa watu baada ya picha kuzagaa mitandaoni ikimuonesha akiwa nchini nchini Malaysia na aliyekua mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu ambaye pia ni muigizaji wa filamu za kitanzania. Picha zikiwaonesha wawili hao wakiwa katika pozi tofauti tofauti za kimahaba na watu kusema wawili wamerudiana na mpenzi wake Diamond (PENNY) alie tu. "Watanzania naomba kutamka wazi, na kuwajuza yote mlioyasikia au kuona katika picha tofauti nikiwa na Wema, niko Malaysia na hizo picha ni katika viande vya movie tunayoigiza iitwayo TEMPTATION hii ni movie itakayochezwa sehemu mbali mbali duniani kwahiyo naomba msiwe mnaongea vitu bila kumuuliza muhusika." Alisema Diamond kwenye account yake ya instagram. |
|
0 comments:
Post a Comment