Mshindi wa Tusker Project Fame All Star 2011, Peter Msechu pichani kushoto pamoja na Malkia wa kiwanda cha filamu Bongo, Wema Issack Sepetu kwa pamoja wameamua kuwa pamoja ili kuweza kusogeza kurudumu la maendeleo katika tasnia hii ya Filamu Bongo. Wakiongea kwa pamoja wakati wakiwa Location walisema wameamua kufanya hivyo kwani wao kwa pamoja wamepata mkataba wa pamoja na kampunu moja ya usambazaji fialmu Tanzania. "Kiukweli najisikia raha sana kufanya filamu na mrembo kama huyu maana hii kitu ilikua kwenye moja ya ndoto zangu na namshukuru Mungu zinaenda kutimia" alisema Peter Msechu. " Kiukweli Msechu anajua sana kuigiza hata mimi nimejisikia raha kuigiza na Msechu maana kweli jamaa ana kipaji cha uigizaji" Peter Msachu na Wema wameshiriki kwa pamoja filamu iitwayo "CRAZY TERNAT" |
0 comments:
Post a Comment