Icon wa kiwanda cha filamu Bongo, Haji Adam (Baba Haji) a.k.a the People's choice juzi kati ameingi a kwenye mkosi baada ya kutapeliwa kiasi cha zaidi ya sh. 200,000/= ikiwa ni malipo ya mwisho ya filamu aliyokuwa akiiongoza. Filamu ijulikanayo kama "NEW DILLEMA" Baba Haji amehusika vizuri katika kuiongoza lakini kampuni iliyomuajiri kuongoza filamu hiyo (jina tunalo) ilimuambia baba haji kuwa asubiri kidogo maana fedha ziliwaishia, ndipo Baba Haji akaamua kutumia ustaarabu wa kusubiri mpaka siku inayofuata. Cha kushangaza siku inayofuata Boss wa kampuni hiyo na wenzake wakataka kutoroka bila hata kuwapa taarifa wasanii na Director (Baba Haji) ndipo msamaria mwema akaamua kuwatonya akina Baba Haji na wenzake kuwa wanatapeliwa ndipo wakaamua kuwachulia sheria mkononi. Ndugu mfuatiliaji wangu nitakujuza kila kitu kilichofuata baada ya hapo. |
0 comments:
Post a Comment