Baadhi ya watu huamini kua mrembo ni lazima uwe mweupe au ni lazima uwe na kipato kikubwa ili uweze kununua baadhi ya vitu kujipendezesha. Ukweli ni kwamba, rangi ambayo Mwenyezi Mungu amekupa na hali uliyokua kimaisha inaweza kabisa kwa asilimia zote kukufanya wewe uonekane mrembo na wa kuvutia kabisa. Sababu kubwa ya kukufanya wewe uonekane mrembo ni Usafi, Kujiamni, Kujiheshimu, nakatika kujiheshimu ni pamoja na mavazi unayovaa. Unapswa kujua vazi gani ni la usiku, vazi gani ni mchana, vazi gani ni ufukweni na vazi gani la kushindia nyumbani. |
|
0 comments:
Post a Comment