Icon wa Bongo Fleva Tanzania, Naseeb Abdul Juma (Diamond Platnumz) amesheherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa hana raha kabisa baada kuuguliwa na mama yake mzazi. Akizungumza kwa huzuni na upole sana alipokua akiongea na mdau wangu, Diamond amesema kua kiukweli mama yake ndiyo kila kitu kwa hiyo ugonjwa alionao mama yake unampa huzuni sana kwani mama yake ndiyo kila kitu katika maisha yake. ''Kiukweli mama yangu ndiyo hua ananiongoza kwenye mambo yangu mengi sana so ninapomuona anaumwa naona kama mambo yangu yatakwama sana.'' Mama wa mwana bongo fleva anasumbuliwa na malaria lakini mpaka naandika habari hii alikua akiendelea vizuri. |
0 comments:
Post a Comment