Msanii ghali kwa sasa Tanzania, Naseeb Abdul Juma (DIAMOND) yuko nchini Uingereza na Meneja wa kundi la The Fuse katika kusaini mkataba wa kimataifa wa kuanza kuuza nyimbo zake kama Caller tune nchini humo Uingereza. Diamond anaamini kuna Watanzania wengi walioko nje ya Tanzania ambao huitaji sana kupata nyimbo zake na za Watanzania wengine lakini hawajui jinsi ya kuzipata. Tumuombee Mtanzania mwenzetu kwani hatua anayopiga ni kubwa na awape na wasanii wengine mianya ya kuweza kufika hapo alipo na azidi kusonga mbele na asitosheke na mafanikio madogo aliyopata kwa sasa. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Naseeb Abdul. |
Tuesday, May 7, 2013
DIAMOND PLATNUMZ KUUZA UINGEREZA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment