TANGAZO

KWA WALE WANAOHITAJI T.SHIRT KWAAJILI YA SARE SIKU YA AMBAYO WASANII WATAJUMUIKA KWA PAMOJA SIKU YA KWENDA MAHAKAMANI WAFIKE BAJOMBA CO.LTD MAGOMENI MOROKO HOTEL AU WAPIGE SIMU NAMBA:0715316796. BILA KUSAHAU MCHANGO WA TSH. 2000/=

Wednesday, October 9, 2013

UKWELI NDIO HUU......



Galacha wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Juma, Diamond ameingia tena vinywani mwa watu baada ya picha kuzagaa mitandaoni ikimuonesha akiwa nchini nchini Malaysia na aliyekua mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu ambaye pia ni muigizaji wa filamu za kitanzania. Picha zikiwaonesha wawili hao wakiwa katika pozi tofauti tofauti za kimahaba na watu kusema wawili wamerudiana na mpenzi wake Diamond (PENNY) alie tu. "Watanzania naomba kutamka wazi, na kuwajuza yote mlioyasikia au kuona katika picha tofauti nikiwa na Wema, niko Malaysia na hizo picha ni katika viande vya movie tunayoigiza iitwayo TEMPTATION hii ni movie itakayochezwa sehemu mbali mbali duniani kwahiyo naomba msiwe mnaongea vitu bila kumuuliza muhusika." Alisema Diamond kwenye account yake ya instagram.

I REAL LOVE MY PENNY SIJARUDIANA NA WEMA-DIAMOND

Ni maneno ya nguli wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul Juma 'DIAMOND PLATNUMZ' kua anawashangaa watu wanaovumisha kua amerudiana na aliyekua mpenzi wake wa zamani Wema Isack Sepetu, 'Madam'  "jamani kwani watu wakiachana ndio wasiongee? Ukiachana na mtu hakuna haja ya kua na uadui au sababu alicomment kwenye account yangu ya Instagram? Jamani tubadilike ukiachana na haimaaniishi kua muwd maadui" alisema Diamond kwenye ukurasa wake wa facebook.. "I REAL LOVE MY PENNY NA SIJARUDIANA NA WEMA"

Diamond akiwa na mpenzi wake Penny, siku wakisheherekea siku ya kuzaliwa kwa Diamond.


Monday, October 7, 2013

DIMOND AZUNGUMZIA WANAOM-COPY NA KUMUIMBA VIBAYA.

Mwanamuziki ghali kuliko wote Tanzania, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' Anayetamba na wimbo wa MY NUMBER ONE, amesema wako vijana wanao jaribu ku-copy nyimbo zake na kuziimba sio kitu kibaya lakini ni vyema wakakaa chini na kuumiza vichwa na kutunga nyimbo nzuri watasikika tu kuliko kusubiri yeye atoe wimbo na wao ndio waimbe. Akizungumza kwa simu Diamond ambaye pia ni mchumba wa Mtangazaji Penny, amesema siri kubwa ya mafanikio yake ni kujituma na kumuomba Mumgu sana, kitu ambacho hata hao wanao muiga wakifanya hivyo watakua kama yeye au hata zaidi. Diamond amesisi tiza kua kwa sasa yuko studio kurekodi wimbo mpya kwaajili ya mashabiki wake. "niko studio nawaandalia ngoma kali is not easy kwa kweli" alisema Diamond. Blog hii inamtakia kila la kheri kwa kile anachokifanya na Inshallah Mwenyezi Mungu atamfikisha mbali katika kuitangaza Tanzania kimataifa.

Wednesday, October 2, 2013

MAMA HUYU ANAOMBA MSAADA AKATIBIWE INDIA.

Watanzania  wenzangu mama huyu anahitaji msaada wa hali na mali ili aweze kwenda India katika hospitali ya Apolo kuweza kutibiwa mguu uliomvimba. Kwa yeyote atakayeguswa na tatizo hili atoe mchango wake kupitia account namba 011201364730 NBC. Kinahitajika kiasi cha shilingi milioni 19. Kutoa ni moyo na si utajiri. Matatizo ni kwa kila mtu leo kwangu kesho kwako.

Monday, September 30, 2013

MAPOKEZI YA DIAMOND PLATNUMZ ZANZIBAR, MPAKA KWENYE SHOW.

AKIWA AMESALI UWANJA WA NDEGE...

AKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI MUDA MCHACHE KABLA YA SHOW...

MASHABIKI WA DIAMOND WALIOJITOKEZA KUMLAKI...


AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KABLA YA SHOW...


WASAFI CLASSI BABY (WCB) KAMA WENYEWE WANAVYOJIITA WAKIWAJIBIKA JUKWAANI HUKO ZANZIBAR...





















VIDEO ALSHABAB WALIPOVAMIA JENGO LA BIASHARA KENYA (WESTGET)


KWAHERI GRACE MBOWE.

Marehemu Grace Mbowe, (kushoto) na pichani ni siku ambayo alijiunga na Chama tawala (CHAMA CHA MAPINDUZI) lakini hivi sasa ni marehemu. Grace amefariki kwa ajali ya gari yeye na mumewe wakiwa safarini kuelekea Dar-es-Salaam, maeneo ya Segera ambapo umauti uliwafika mda mchache wakiwa hospitali.